MAJERAHA YA NAFSI – UTANGULIZI
Kuna majeraha ya mwili na Majeraha ya
nafsi.
Hapa sisemi habara za Majeraha au
Vidonda vya ndani ya mwili bali nafsini.
Nafsi kwa sehemu kubwa ni jambo la
kiroho; hivyo watu wanapata ugumu mkubwa kuelezea mambo ya nafsi maana ufahamu
wa mwilini hawezi kuelezea mambo ambayo ni ya rohoni.
Kimsingi Mungu aliumba mwanadamu
akawa na vitu vitatu; Mwili, Nafsi na
Roho. Roho na Nafsi ni vitu vigumu kueleweka kwa jinsi ya mwilini ila
vinaeleweka kwa jinsi ya rohoni. 1Wathesalonike
5:23. Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi
kabisa, roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, nanyi mhifadhiwe kikamilifu bila
kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. kwa mujibu wa maneno hayo inathibitisha kuwa mtu ni
roho,nafsi pamoja na mwili. Ikiwa kasema “Tukaze nafsi” mwili na roho zetu
maana yake yote yaani nafsi,Mwili, na Roho vinaweza vikapata shida ikiwa kuna
mazingira vikipitishwa kama Mungu anataka kutakasa nafsi zetu, maana yake
anataka kuziponya nafsi zetu, kwa hiyo nafsi inaweza ikapata vidonda.
Ukisoma Zaburi 55:4, inasema Moyo wangu unaumia ndani yangu na hofu za
maiti zimenizunguka.
Moyo wake au nafsi yake inaumia na
asikia ndani yake maumivu na hayo maumivu yamejenga hofu ndani ya moyo wake.
Siku zote Majeraha ya Nafsi
huwayanajenga mfumo wa maisha, kwa mfano:
Zaburi 55:4 Majeraha yake ya Nafsi yalimjengea hofu au mfumo wa kuishi kwa
Uoga. Hofu si mfumo pekee ambao Majeraha
ya Nafsi yanajenga, ipo mifumo mingi na
ambayo hipo kinyume na mfumo wa Ufalme wa Mbinguni.
Mathayo 6:12
Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi
tulivyokwishakuwasamehe wadeni wetu.
Mfumo wa maisha ya mbinguni unatutaka
kuwasamehe wale waliotukosea na kutusababishia Majeraha ila mtu aliyejeruhiwa Moyo utamjua kuwa ni
mgumu kwenye kusamehe maana anaona aliyemkosea hastahili kusamehewa; lakini
swali la kujiuliza ni nani katika Wanadamu ambaye amesamehewa na Mungu kwa
kusahili? Jibu ni wazi kuwa “Hakuna|”
Ugumu wa kutokusamehe unasababishwa
na uchungu, lile fundo la uchungu lililokaa ndani ya moyo kishelia ni uchafu
ndani ya moyo;
Maana Biblia inasema Takaseni Nafsi
zenu hivyo Wathesolomike 5:23 uondoe
uchafu wa moyo ikiwemo uchungu.
Mtu aliyejeruhiwa Moyo maana yake pia
amekosa “AMANI” na Mwanadamu
hakuumbwa kuishi bila kuwa na Amani kwa hiyo itambidi atafute Amani kwa gharama
yeyote ile, au kitu chochote atachofanya na kitampa Amani. Kina Amani za aina
nyingi lakini si kila tendo linaweza kumpa Amani ya kweli.
Kina Amani ya Dunia.
Yohana 14:27
“Amani nawaachieni; Amani yangu
nawapa niwapavyo mimi sivyo kama Ulimwengu utoavyo.
Hapa tunaona kina Amani ambayo Kristo
anampa mtu na kuna Amani ambayo Ulimwengu unapaswa watu, ni Amani zenye uwezo tofauti ila yenye nguvu
ni Amani ya Kristo Yesu.
Badala ya kuingia kwenye vilevi ;
kama pombe ili kupata ‘Amani” ni bora ujazwe Roho. Tusilewe kwa mvinyo bali
tujazwe Roho ndivyo ushauri wa Biblia.
Ndani ya Roho Mtakatifu kuna Amani ya
Kristo inayopita fahamu zote na kuhifadhi mioyo yote Wafilipi 4:6-7
Na Amani ya Mungu ipitayo alali zote,
itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Maana ya majeraha ya nafsi.
Tumeona kuwa Majeraha ya Nafsi
yanajenga mfumo wa maisha ambayo ni kinyume kabisa na ule wa Ufalme wa
Mbinguni.
Kwa kujeruhiwa na ama kujijeruhi wewe
mwenyewe katika mapito unayopita katika maisha yako ya kila siku. Si kila mtu
kajeruhiwa wengine wamejijeruhi wenyewe.
Ukiona kuna jambo ulifanya hata kama
ni kipindi cha nyuma lakini ukilikumbuka kama unasikia kulipa kisasi au moyo
kuinama au uchungu au unaona hata bora unge…….ujue hiyo ni ishara ya jeraha la
nafsi.
Zaburi 39:1-3
Moyo wangu ukawa moto ndani, na
katika kuwaza kwangu moto ukawaka; Nilisema kwa ulimi wangu.
Kama aliwaza au kama alikumbuka na
moto ukawaka ndani yake maana yake alipokuwa akiwaza akawa anasikia uchungu
“Yaaani kwanini nitendewe hivi au vile”
Kama kuna mtu unamkumbuka na kasha
unalia au unasikia uchungu ni ishara ya kujeruhiwa moyo.
KAMA UNA MAJERAHA YANAFSI NA UNAHITAJI
KUFUNGULIWA ,BASI TAMKA MANENO YAFWATAYO KWAIMANI
NAWE UTAPOKEA UPONYAJI.
Waebrania 11:1-3,Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni
udhahiri wa mambo yasiyoonekana. 2Naam, kwa imani baba zetu wa kale
walishuhudiwa.
3Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu
vyote vinavyoonekana viliumbwa kwa vitu visivyoonekana.
MAOMBI YA KUTAMKA
Hee MUNGU muumba wa mbingu na nchi kwajina la yesu kristo mnazareti kupitia roho mtakatifu ,naomba nisamehewe dhambi
nilizofanya katikamaishayangu, kwamatendo ,maneno na katika kuwaza kwangu
kwajina la yesu kristo kupitia roho mtakatifu.Ninakataa na kuharibu kumbukumbu za mambo mabaya katika fikra na
moyo wangu. Maumivu yote katika moyo
wangu yatoweke katika jina la yesu
kristo kupitia roho mtakatifu ,na damu ya yesu
ifunike moyowangu na maisha yangu katika jina la yesu
kristo kupitia roho mtakatifu. Maagano yote ya nguvu zagiza yaliyo wahi
kufanyika ama kwa kujua au kwakutokujua nayaharibu katika jina la yesu kristo kupitia roho mtakatifu ,Bwana yesu futa jialangu katika kitabu cha
ukumu na uandike katika kitabu cha uzima amen.
BY MAUMA’MSYANGI ELIKANA (MTUMISHI PAUL MAUMA)
DODOMA –TANZANIA
TEL:0756319013